المدة الزمنية 7:18

Gari la Kishetani Lililochukua Roho za kila aligusalo

بواسطة Uswaziflix
73 مشاهدة
0
2
تم نشره في 2020/10/11

Majanga yanaanzia Septemba 23, 1955, ambapo James Dean raia wa Los Angeles US alinunua gari yake ya michezo aina ya Porsche 550 kwa muuzaji George Barris na akaenda kuiboresha zaidi ionekane vile alivyokuwa anapenda yeye iwe. James aliweka siti mpya nzuri ya tartan, akaandika namba 130 ubavuni, na kwenye injini alikuta yameandikwa maneno 'Little Bastard', haya yaliandikwa na George mwenyewe aliyekuwa mmiliki wa kwanza wa gari hilo kabla James hajanunua,maneno yale hayakumpendeza hivyo Akayafuta. Siku hiyo hiyo Septemba 23, 1955, wakati James akiendesha gari lake karibu na Los Angeles, alikutana na muigizaji wa Alec Guinness nje ya mgahawa mmoja, akaombwa apande lakini Alec alikataa huku akionyesha hofu na uwoga mkubwa. Siku iliyofuata ikabidi amwandikie barua James kueleza ni kwanini alikuwa akionyesha hofu kupanda kwenye gari lake. "Gari lako lilionekana kuwa baya sana kwangu, lilinipa shida, hasira, nikahisi kuumia sana. licha ya fadhili zako lakini nilijisikia mwenyewe nikisema kwa sauti ambayo sikuweza kabisa kuitambua kama ni sauti yangu, iliniambia 'tafadhali usiingie kamwe ndani ya gari, utakua maiti ndani ya wiki" Baada ya James kusoma barua hii ya Alec, akacheka tuu kwa dharau. Wiki moja baadaye Septemba 30, James na wenzake walikuwa wakifanya mazoezi ya kukimbiza magari kwani gari lake pia ilibidi likatumike katika mashindano ya mbio za magari huko Salinas California mwishoni mwa juma hilo. Ni kweli mazoezi yalianza kufanyika, lakini kwa bahati mbaya James alipata ajali mbaya kwa gari lake kugongana na gari jingine na kufariki papo hapo, yule muuzaji wa gari George akaja tena kununua 'skrepa' za gari hilo baada ya kutokuwa na uwezo wa kutengenezeka tena, ukizingatia na mmiliki wake James tayali alishafariki.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 0