المدة الزمنية 58:15

KKKT USHARIKA WA KIJITONYANYA IBADA YA SIKU YA JUMAPILI 19/ 07/ 2020

7 923 مشاهدة
0
119
تم نشره في 2020/07/19

KKKT USHARIKA WA KIJITONYANYA IBADA YA SIKU YA JUMAPILI 19/ 07/ 2020 "MARAFIKI WANNE WENDAWAZIMU" "FOUR CRAZY FRIENDS" ( THE IMPACT OF CRAZINESS OR MADNESS IDEAS ) Marko 2 : 1 - 12 Mhubiri 9 : 3 Marko 2 : 1 - 12 Marko 2:1 (SUV) 1 Akaingia Kapernaumu tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani. Marko 2:2 (SUV) 2 Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake. Marko 2:3 (SUV) 3 Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne. Marko 2:4 (SUV) 4 Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza. Marko 2:5 (SUV) 5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako. Marko 2:6 (SUV) 6 Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao, Marko 2:7 (SUV) 7 Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu? Marko 2:8 (SUV) 8 Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu? Marko 2:9 (SUV) 9 Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende? Marko 2:10 (SUV) 10 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza), Marko 2:11 (SUV) 11 Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako. Marko 2:12 (SUV) 12 Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe. Mhubiri 9 : 3 Mhubiri 9:3 (SUV) 3 Baa hilo ni katika mambo yote yanayofanyika chini ya jua, ya kuwa wote wanalo tukio moja; naam, zaidi ya hayo, mioyo ya wanadamu imejaa maovu, na wazimu umo mioyoni mwao wakati walipo hai, na baadaye huenda kwa wafu. Mhubiri : Rev. Dr. Eliona Kimaro Kwa maombi na ushauri: Mch. Dkt. Eliona Kimaro. Simu :+255655516053, +255754516053 YouTube : Rev. Dr. Eliona Kimaro TV Barua Pepe: elionakimaro555@gmail.com

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 34