المدة الزمنية 10:52

EXCLUSIVE: UJUMBE ULIOANDIKWA NA MAALIM SEIF KWA WANAMAGEUZI/ULIPOKELEWA UFUKWENI

بواسطة MwanaHALISI TV
10 417 مشاهدة
0
42
تم نشره في 2021/02/17

James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi ameeleza namna Maalim Seif Shariff Hamad alivyokuwa mstari wa mbele katika mageuzi. Amesema, licha ya kuweka gerezani wakati wa vuguvugu la mabadiliko, alituandikia ujumbe wake kwa wanamageuzi kututia moyo wa kusonga mbele. "Nimemfahamu Maalimu kwa zaidi ya miaka 29, wakati tunaanzisha mageuzi mwaka 1991 mwezi wa sita, yeye alikuwa gerezani lakini aliandika salaam zake kwetu kutupa moyo, alivyotoka gerezani nilienda kuishi kwake," amesema. Mbatia amesema, Maalim Seif aliishi kile anachokiamini, hivyo ameacha somo la kutokata tamaa. "Aliishi kile alichokiamini, mpaka mauti yanamkuta hakukata tamaa. Alikuwa mkweli wa maneno na vitendo. 🔘JE, NA WEWE UNA HABARI? 🔘WASILIANA NA MwanaHALISI TV ( +255 767 400402), 🔘WhatsApp ( +255 692 318213) 🔘Email: mwanahalisitvnews@gmail.com 🔘KWA HABARI ZA KILA SIKU: http://mwanahalisionline.com

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 7