المدة الزمنية 2:36

TCRA:Kuhusu utapeli kwenye simu.

بواسطة Buha TV Online
94 مشاهدة
0
2
تم نشره في 2023/07/18

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imetoa  wito kwa  jamii kuwa na kumbuku na watu ambao waliwasajilia laini za simu kwa kutumia kitambulisha cha nida maana wanaofanya utapeli ni watu wao wa karibu .. Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabir Bakari alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA na maendeleo. Aidha amesema kuwa mafanikio yaliyofanywa na Mamlaka hiyo ni pamoja na nchi kuweka jitihada ya kupunguza data kwa Gb kuliko nchi yoyote ya afrika mashariki. TCRA ilianzishwa chini ya Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Namba 12 ya mwaka 2003 baada ya kuunganishwa kwa iliyokuwa Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC)  na Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC).

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 1